Wednesday, September 16, 2015

Drake ahudhuria maonyesho ya mitindo ya mavazi kumuunga mkono Serena Williams

 
 Baada ya kuonekana kumuunga mkono Tennis star Serena Williams kwa kumshanglia kwa nguvu katika mashindano ya mpira wa tennis ya U.S Open hivi karibuni,rappa Drake kwa mara nyingine ameoneka kumuunga mkono Serena baada ya kuhudhuria na kukaa siti za mbele kabisa katika maonyesho ya mitindo ya mavazi ya Serena Williams ikiwa kama sehemu ya maonyesho ya New York Fashion Week jana siku ya jumanne.
Wanamitindo walitembea jukwaa huku katika spika zikisiskika nyimbo mbali mbali za Drake zikiwemo “Hotline Bling,”“My Love” na “Ojuelegba,” aliyoshirikikishwa na msanii toka Africa,mnaijeria Wizkid.
Drake pia alionekana akiwa na Serena backstage akimpongeza kwa furaha na mabusu mkononi.

Drake pia alionekana amekaa siti za mbele na Anna Wintour ambaye ni editor in chief wa jarida la  Vogue baadaye picha hiyo ikatumwa mtandaoni ikiwa na caption “Me and bae.”

No comments:

Post a Comment