Monday, September 21, 2015

Treach apinga usemi wa waliohit hawatong'aa tena

Treach Refutes Claim That Hit-Makers Can't Battle Rap 

Star wa Naught By Nature,Trech anapingana na usemi usemao,ivumayo aidumu ama waliong'ara aali hawatong'aa tena.
Akiongea katika mahojiano na mwandishi wa mtandao wa AllHipHop aliwazungumzia mastaa waliong'ara  kama Keith Murray na Fredro Starr  kwamba watashiriki katika project ya  MC WAR’s “Generation X” eventTreach amesema kwama hit-makers hao wana nafasi sawa na wanauwezo wa kuwa na mafanaikio awa ama zaidi ya hawa walioko sasa.

“Usually they say battle emcees can’t make hit records. Now we’re gonna show how those emcees that made hit records can battle,” Treach explained. "My prediction is, who going to win this battle, whoever got the hottest lyrics."
Akimaanisha: wanasema ma Mc wa vilingeni ( battle emcees ) si rahisi kufanikiwa kufanya ngoma kali,sasa tutawaonyesha namna gani hawa ma Mc watakavyotoka na ngoma kali na katika mpambano huu mshindi ni Mc mkali wa mistari.
Mpmbano wa nne wa MC WAR event umepangwa kufanyika hukoBrooklyn’s Milk River tarehe 4 mwezi October.

Rick Ross amvisha pete ya uchumba mpenzi wake,Lira Mercer


Rick Ross mwenye umri wa miaka 39,amefanya kweli.Rappa huyo ambaye hana skendo za masuala ya mahusiano,amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake ambaye awali alikuwa m burudishaji wa club za usiku ( stripper ) Lira Mercer 22.
Aka Mercer,Lira Galore,aliweka katika mitandao habari na picha ya kuwa amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa sasa,Rick Ross akionyesha pete yake ya almasi ya thamani.

Mercer ameshatajwa kujihusisha kimapenzi na mstaa kibao wakiwamo Diddy, Drake,Justin Bieber na wengine lakini bosi huyo wa MMG hajaangalia hayo yote amefuata moyo wake unataka nini.
Na katik habari nyingi kuna yanayosemkana kwamba mama wa mremboLira amesema hajali minong'ono kuwa mchumba wa mwanawe ana wanawake wengine alimradi amemvisha pete ya almasi.

Friday, September 18, 2015

Rihanna & Snoop Dogg miongoni mwa waliotwajwa kuongoza kwa ubora wa picha binafsi "Selfies"

 
Mitandao ya kijamii imekuja na mambo mengi.Ukiachilia mbali watu kupata uhuru na wepesi wa kujitangaza kwa haraka pia mengi mazuri kwa wenye matumizi mazuri na mitandao hiyo.
Mara hii kimekuj kitu kipya kinachofahamika kama “The Greatest Celebrity Selfies Of All Time.”
Picha ya Rihanna aliyojipiga binafsi huko kwao Barbados mi moja kati ya zilizomo katika  zilizotajwa.Moja kati ya sababu zilizopelekea picha ya Rihanna aliyopiga katika tamasha la Crop Over festival,kuingizwa katika orodha ya “The Greatest Celebrity Selfies Of All Time.” ni mapenzi ya star huyo kwa nchi yake hiyo.
Snoop Dogg aliingizwa katika orodha hiyo baada ya picha yake ya kituko ya “Pancake Face” .
"This image makes this list because it combines three things that are very important to the Internet: food, emojis, and Snoop Lion,” the story says. "His name may change, but his pancake face selfie is forever.”
  celebrity selfies  

Thursday, September 17, 2015

T.I. aongelea kuacha kufanya kazi na Iggy Azalea

 T.I. Explains Parting Ways With Iggy Azalea
Rappa T.I.P. alifanyiwa mahojiano na kipindi cha Ebro in the Morning na waliongelea mada mbali mbali zikiwemo kubadili jina lake kutoka T.I mpaka T.I.P,muziki wake mpya mpaka mahusiano yake na rappa wa kike,Iggy Azalea.
Kuhusu Iggy, T.I. alianz auona dalili za kutokuwa sawa tangu kipindi alipokosolewa kuhusu miiko ya Hiohop na Legendaru rappa Q-Tip,kwani T.I anasema kama Iggy alilalama kwamba hakuwa upamndewake kumtetea kama msanii wake japo alijisahau kwamba alimkingia kifua pindi wanarushiana maneno na vijembe na Snoop Dogg. 
T.I ambaye sasa anafahamika kama T.I.P amesema alivyoona dalili za Iggy kuondoka na kutaka kufanya mambo yake hakuwa na jinsi ya kumzuia kwani anaamini amefanya smart movo na atakuwa sawa huko aendako kwani ana kipaji,Tip piaameongza kusema hakuwa na muda wa kupoteza zaidi na Iggy labda wayaweke sawa kwani  kwasasa yupo bize akipika albamu yake ya 10 studio.
The rapper also found his way to dodge the recent Drake and Meek Mill beef wanting nothing to do with that beef.

50 Cent awachana BET & The Emmys kuhusu kutangaza orodha ya wanaowania


 50 Cent Blasts BET & The Emmys For Nomination Snubs
Kama ilivyo bongo,malalamiko na minong'ono huwa haikoseknani either iwe katika kutajwa wanaowania tuzo ama walioshinda tuzo hizo na America vivyo hivyo.Baada ya kituo cha televisheni cha BET kutaja majina ya wanaowania tuzo za BET Hip Hop Awards50 Cent 2015,rappa na bosi wa G-Unity,50 Cent amwajia juu na kuwachana waandaaji wa tuzo hizo haswa katika kipengele cha Video Director of the Year baada ya Eif Rivera,ambaye ameongoza video ya bosi huyo wa the G-Unit ' "9 Shots" video,kutotajwa kuwania tuzo hiyo.
Kupitia akaunti yake ya Tweeter 50 Cent aliandika: "Director of the Year, 👀 where the fu😡k is Eif Rivera?" aliandika maneno hayo chini ya pich yake na Rivera wakiwa na kitita cha pesa  na kuongeza kuandika: "You have the same list ever year. "
Wanaowania tuzo kipengele cha Video Director of the year mwaka huu ni Alan Ferguson, Benny Boom, Chris Robinson/Lil Chris, Colin Tilley and Director X. wakati mwaka jana waliowania ni Benny Boom, Chris Robinson, Director X, Dre Films na Hype Williams ambaye mwaka huu hakutajwa lakini alichukua tuzo hiyo mwaka jana.

Sherehe za utoaji tuzo za 10 za BET Hip Hop Awards zimepangwa kufanyika October 13.

Wednesday, September 16, 2015

Lil Wayne amefunguliwa kesi ya madai yadolla milioni 2 na kampuni ya Private Jet

Lil Wayne Sued For $2 million By Private Jet Company

Lil Wayne imetangazwa anadaiwa kiasi kisichopungua dolla millioni 2 kama malipo ya miaka mitatu  ambayo hajailipa kampuni ya wakodishaji wa ndege za kifahari za private jet.
Kampuni hiyo mwezi August mwaka 2014 walimfungulia mashataka Li Wayne kwamba wanamdai dolla millioni 1 na walishinda kesi.
Msemaji wa kampuni hiyi inayofamhamika kama Signature Group amesema pamoja na mahakama kusema wameshinda kesi Lil Wayne hakuwalipa hivyo gharama zimeongezeka kama dola 800,000  na hivyo kufikia dolla millioni 2.
Lil Wayne and Young Money pia wapo matatni katika madeni mbalimbali yakiwemo mamilioni ya mauzo ya tiketi za maonysho waliyoshindwa kuhudhuria.

Fahamu kinachomuingizia mkwanja mwingi Michael Jordan kuliko pesa aliyopata akicheza kikapu

 
Michael Jordan ametengeza mkwanja wa kutosha.
Akichukuliwa kama moja kati ya wachezaji wakubwa na waliong'ara zaidi katika ligi ya mpira wa kikapu marekani NBA,Michael Jordan pia ni moja kati ya wachezaji wa mpira huo waliojiingizia mkwanja zaidi.
Mtandao wa PBS umepost habari za kushtua kuhusu kiasi gani MJ alijiingizia akiwa anacheza mpira wa kikapu na imeshangaza kuona Jordan alijiingizia kiasi cha dolla millioni 94 katika kipindi cha miaka 15 lakini amejiingizia zaidi ya dolla millioni 100kwamaka jana tu kupitia mauzo ya nguo,raba na mavazi mbalimbali yenye nembo za Jordan .

Drake ahudhuria maonyesho ya mitindo ya mavazi kumuunga mkono Serena Williams

 
 Baada ya kuonekana kumuunga mkono Tennis star Serena Williams kwa kumshanglia kwa nguvu katika mashindano ya mpira wa tennis ya U.S Open hivi karibuni,rappa Drake kwa mara nyingine ameoneka kumuunga mkono Serena baada ya kuhudhuria na kukaa siti za mbele kabisa katika maonyesho ya mitindo ya mavazi ya Serena Williams ikiwa kama sehemu ya maonyesho ya New York Fashion Week jana siku ya jumanne.
Wanamitindo walitembea jukwaa huku katika spika zikisiskika nyimbo mbali mbali za Drake zikiwemo “Hotline Bling,”“My Love” na “Ojuelegba,” aliyoshirikikishwa na msanii toka Africa,mnaijeria Wizkid.
Drake pia alionekana akiwa na Serena backstage akimpongeza kwa furaha na mabusu mkononi.

Drake pia alionekana amekaa siti za mbele na Anna Wintour ambaye ni editor in chief wa jarida la  Vogue baadaye picha hiyo ikatumwa mtandaoni ikiwa na caption “Me and bae.”

Majina ya wanaowania tuzo za BET Hip-Hop 2015 yatajwa,rapa Drake aongozwa kutajwa

 Drake
Mchakato wa tuzo za kituo cha televisheni cha BET,BET Hip-Hop awards 2015 umeanza kwa kituo hicho kutangaza majina ya waliongia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hizo.Rappa toka Toronto huko Canada,Drake ametajwa kuongoza kutajwa mara nyingi kuliko wote wanaowania tuzo hizo kwa kutajwa mara 12.
Drake ametajwa kuwania tuzo zikiwemo za Best Live Performer, Lyricist of the Year, MVP of the Year, Album of the Year, Hustler of the Year na kama haitoshi featured artist in Best Hip-Hop Video, Best Collabo, Duo or Group na People’s Champ Award.
rapa toka Good Music,Big Sean anamfuatia kwa kutajwa mara 10 huku rapa wa kike Nicki Minaj akitajwa mara 9.Kendrick Lamar na J. Cole wao wametajwa kuwania tuzo hizo mara 8.
Sherehe hizo za utoaji wa tuzo za za hiphop za BET 2015 zitaongozwa na legendary rappa Snoop Dogg na zitafanyika Oct. 9 kutoka katika ukumbi wa the Boisfeuillet Jones Atlanta Civic Center huko Atlanta na zitaonyeshwa sambli usiku Oct. 13.


Tazama majina ya na vipengele vya wanaowania tuzo za BET Hip-Hop Awards 2015.
Best Hip-Hop Video
Big Sean feat. Chris Brown and Ty Dolla $ign – “Play No Games”
Big Sean feat. Drake and Kanye West – “Blessings”
Fetty Wap – “Trap Queen”
Kendrick Lamar – “Alright”
Nicki Minaj feat. Beyoncé – “Feeling Myself”

Best Collabo, Duo or Group
Big Sean feat. Drake and Kanye West – “Blessings”
Big Sean feat. E-40 – “IDFWU”
Fetty Wap feat. Monty – “My Way”
Nicki Minaj feat. Beyoncé – “Feeling Myself”
Nicki Minaj feat. Drake and Lil Wayne – “Truffle Butter”

Best Live Performer
Drake
J. Cole
Kanye West
Kendrick Lamar
Nicki Minaj

Lyricist of the Year
Big Sean
Drake
J. Cole
Kendrick Lamar
Nicki Minaj

Video Director of the Year
Alan Ferguson
Benny Boom
Chris Robinson/Lil Chris
Colin Tilley
Director X

DJ of the Year
DJ Drama
DJ Envy
DJ Esco
DJ Khaled
DJ Mustard

Producer of the Year
DJ Mustard
J. Cole
Kanye West
Mike Will Made-It
Pharrell Williams
Timbaland

MVP of the Year
Big Sean
Drake
Future
J. Cole
Kendrick Lamar
Nicki Minaj

Track of the Year
“Alright” – Produced by Pharrell Williams and Sounwave (Kendrick Lamar)
“Blessings” – Produced by Boi-1da and Vinylz (Big Sean feat. Drake and Kanye West)
“Commas” – Produced by DJ Spinz and Southside (Future)
“IDFWU” – Produced by Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West and Key Wane (Big Sean feat. E-40)
“Trap Queen” – Produced by Tony Fadd (Fetty Wap)

Album of the Year
Big Sean – Dark Sky Paradise
Drake – If You’re Reading This It’s Too Late
J. Cole – 2014 Forest Hills Drive
Kendrick Lamar – To Pimp A Butterfly
Nicki Minaj – The Pinkprint
Wale – The Album About Nothing

Who Blew Up Award
Bobby Shmurda
DeJ Loaf
Fetty Wap
Rae Sremmurd
Tink

Hustler of the Year
Dr. Dre
Drake
J. Cole
Jay Z
Nicki Minaj

Made-You-Look Award (Best Hip-Hop Style)
A$AP Rocky
DeJ Loaf
Drake
Kanye West
Nicki Minaj

Best Club Banger
Big Sean feat. E-40 – “IDFWU” (Produced by Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West and Key Wane)
Dej Loaf – “Try Me” (Produced by Dds)
Fetty Wap – “Trap Queen” (Produced by Tony Fadd)
Future – “Commas” (Produced by DJ Spinz and Southside)
Rich Homie Quan – “Flex (Ooh, Ooh, Ooh)” (Produced by DJ Spinz and Nitti Beatz)

Best Mixtape
Future – 56 Nights
Future – Beast Mode
Future – Monster
Lil Wayne – Sorry 4 The Wait 2
Travis Scott – Days Before Rodeo

Sweet 16: Best Featured Verse
Drake – “Blessings” (Big Sean feat. Drake and Kanye West)
Drake – “My Way (Remix)” (Fetty Wap feat. Drake)
E-40 – “IDFWU” (Big Sean feat. E-40)
Kendrick Lamar – “Classic Man (Remix)” (Jidenna feat. Kendrick Lamar)
Lil Wayne – “Truffle Butter” (Nicki Minaj feat. Drake and Lil Wayne)

Impact Track
Big Sean feat. Kanye West and John Legend – “One Man Can Change The World”
Common and John Legend – “Glory” (From The Motion Picture “Selma”)
J. Cole – “Apparently”
J. Cole – “Be Free”
Kendrick Lamar – “Alright”

People’s Champ Award
Big Sean feat. Drake and Kanye West – “Blessings”
Fetty Wap – “Trap Queen”
Future – “Commas”
Kendrick Lamar – “i”
Rae Sremmurd – “No Type”
Rich Homie Quan – “Flex (Ooh, Ooh, Ooh)”
 

Thursday, September 3, 2015

Mistari ya Eminem yapelekea shule 2 kusimamisha masomo na kijana kukamatwa na polisi

Eminem Lyrics Post Leads To Teenager's Arrest
Kijana wa miaka 15 anashikiliwa na polisi wa California baada ya kukamatwa siku ya jumatatu kwa makosa ya kuandika maneno yaliyochukuliwa kama vitisho vya kigaidi aliyoyatoa katika mistari ya wimbo wa Eminem '' I'm Back'' na kuiweka katika ukurasa wake wa Instagram.
Wimbo ''I'm Back'' Eminem unaelezea tukio la mwaka 1999 la mauaji kwa silaha yaliyofanywa na wanafunzi wawili katika shule ya Columbine High School huko Colorado na kupelekea watu 15 kupoteza maisha.
San Joaquin Memorial High School shule ambayo kijana huyo anasoma na shule yake ya zamani St. Anthony’s Catholic School,walisitisha shughuli za masomo juzi september 1 kufuatia vitisho vya mwanafunzi huyo.
Kijana huyo aliandika: 
"I take seven kids from Columbine, stand ’em all in a line, add an AK-47, a revolver, a nine, a MAC-11 and it oughtta solve the problem of mine" the post read. "And that’s a whole school of bullies shot up all at one time. I’m just like Shady and just as crazy as the world was over this whole Y2K thing."
Wana usalama wamesema walimkamata kijana huyo na kitu kizuri ni kwamba kijana huyo ametoa ushrikiano kwa polisi japo amekana kupost ujumbe huo katika ukurasa wa Instagram ujumbe ambao wanausalama wameupiga picha(screen capture).
Kijana huyo sasa yupo mikononi mwa polisi juvenile detention.
Tazama screenshot hiyo hapo chini:
Eminem Lyrics